Maalim Seif: “Hakuna Uhuru Wa Vyombo Vya Habari Tanzania”

Ikiwa leo ni siku ya Uhuru wa habari duniani, Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF, upande wa Zanzibar amesema hakuna uhuru wa vyombo vya habari huku akisema waandishi wanabanwa sana.

Maalim Seif ameyazunguza hayo leo katika kipindi cha clouds 360 kinachorushwa na Clouds Tv wakati alipoulizwa, “Ikiwa leo ni siku ya uhuru wa habari duniani, Je, anaona kuna uhuru wa habari? Ndipo alipongfunguka na kusema hakuna uhuru huo nchini.

“Hakuna uhuru wa habari kwasababu mnabanwa sana kama waandishi wa habari, hii sheria iliyopitishwa mwaka jana ni sheria hatari sana kwa waandishi wa habari. Mimi msimamo wangu nasema msiwabane waandishi wa habari, mwandishi wa habari kama atahisi katenda ubaya, mpelekeni mahakamani iamue,” amesema Maalim Seif.

“Usimpe waziri uwezo wa kufunga gazeti au chombo chochote, aende mahakamani kama kufunga anafunga kwasababu we need real freedom ya waandishi wa habari katika nchi yetu, waibue mambo, wakosoe serikali waziwazi kabisa, wakikusaidia inakuwa rahisi kujua what happened there unapowabana hawa unawafanya watu wote wawe ‘Yes men’, kwa hiyo nasema poleni sana waandishi wa habari.”

Na Emmy Mwaipopo

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.