LULU AIMBIA MAHAKAMA KUU ‘SIJASABABISHA KIFO CHA KANUMBA

Mahakama kuu ya Tanzania leo imesema kuwa muigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael Lulu ana kesi ya kujibu kuhusu tuhuma za mauaji bila kukusudia. Hatua hiyo imekuja leo baada ya upande wa mashtaka kumaliza kutoa ushahidi toka kwa watu wanne. Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia Steven Kanumba.

Baada ya hapo Lulu alipanda kizimbani na kuelezea utetezi wake kama ifuatavyo:

Nilikuwa nataka kutoka ila marehemu ‘Kanumba’ alinikataza, alikuwa hataki nitoke, nilipomwambia natoka na marafiki zangu alinikimbiza na taulo na mimi nilikuwa naogopa kupigwa, mara nyingi alikuwa ananipiga kila akilewa na sio kwa akili zake, alipoona simu yangu inaita akahisi ni simu ya mwanaume akasema kwanini naongea na simu ya mwanaume mbele yake? Marehemu akaingia uvunguni akatoa panga akasema leo nakuua huku akinipiga na panga kwenye mapaja”, ameelezea Lulu.

Marehemu alianguka mwenyewe na kujigonga kwa nguvu na kuinuka sehemu nyingine alikuwa kama anatapatapa, nilimwambia Seth kuwa Kanumba amedondoka na akajaribu kumuamsha hakuamka akasema anaenda kumuita daktari, alivyosema anaenda kumuita daktari na mimi nikaondoka nikiogopa anaweza akaamka akaanza kunipiga, niliondoka nikawasha gari kuelekea Coco Beach kutuliza akili”.

Nilivyofika Coco beach meseji zilianza kusambaa kuniuliza kuwa nasikia Kanumba amefariki, nikampigia ‘Kidume’ ambaye ni rafiki yake Kanumba kumuuliza Kanumba yupo hospitali gani niende kumuona, akaniambia wewe usije hospitali, niambie uko wapi, tukakubaliana tuonane Bamaga, tulivyokutana Bamaga alikuwa kama anataka kuongea na mimi ghafla wakaja askari kunikamata na kunipeleka Oysterbay polisi, Nilipofika Oysterbay nilikuta watu wengi sana niliyemtambua ni Ray. Nilipomkuta Ray Oysterbay polisi nikajua Kanumba amekamatwa kwa sababu ya makelele niliyokuwa nayapiga kule nikajua watu walisikia. Nilijua Kanumba amefariki nikiwa polisi. Kwa namna yoyote ile mimi sijasababisha kifo cha Kanumba, na mimi ndiye nilieshambuliwa na marehemu kutokana na umbile langu nilikuwa mdogo na alikuwa na uwezo wa kufanya chochote kwenye mwili wangu kwa sababu yeye ndo alikuwa na silaha.

 

JICHOLAUSWAZI TUMETOA UPDATE YA APP YETU DOWNLOAD >BOFYA HAPA< KUIPATA MPYA SASA NA UFURAHIE HABARI MOTO MOTO

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.