kiongozi Wa ACT Aachia Ngazi

Katibu wa Chama ACT-Wazalendo Mkoa wa Mbeya, Bahati Longopa ametangaza kuachia wadhifa huo kwa kile alichodai kutoridhishwa na kitendo cha kuteuliwa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi leo, Longopa, amesema haoni sababu ya kuendelea kuwa kiongozi wa chama hicho kwani kitampa wakati mgumu kuhamasisha wanachama wapya katika uchaguzi mkuu mwaka 2020.

“Nimeamua kwa hiari yangu kuacha nafasi ndani ya chama kwani ukiona viongozi wa juu wanateuliwa kuingia katika Serikali iliyopo madarakani inayoongozwa na chama pinzani, sisi wa ngazi za chini tutapata wapi sauti ya kushawishi wanachama wapya kujiunga na ACT-Wazalendo,”amesema.

Kuhusu kujiunga na chama kingine cha siasa amesema kwa sasa ni mapema mno kuzungumzia hilo kwani ataendelea kukaa pembeni na kutojihususisha kwenye mambo ya siasa huku akitafakari nini cha kufanya.

Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo, Wilaya ya Mbeya, Ally Mbika alisema wamepata taarifa za chini chini, lakini kama chama bado hawajakabidhiwa barua yoyote kutoka kwa kada huyo kutamka kujiuzulu rasmi.

source : Bongo5

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.