Joh Makini: Serikali Isiwe Kikwazo Kwenye Kazi Zetu

0

Rapper mkongwe kutoka A Town, Joh Makini akiwa anawakilisha Weusi, amewatolea uvivu vingozi katika tasnia ya sanaa hapa nchini.

Mkali huyo wa ‘Waya’ amezungumzia juu ya kukosa sapoti kutoka serikalini akisema, “Kwakweli hawatusapoti kabisa yaani wanachukulia vitu kikoloni mno, unaweza ukawa unataka kushoot kwenye location ambazo zipo chini ya serikali lakini complicated man, utaambiwa leta barua fanya hivi nafikiri haya ni matatizo ya kuwa na wazee wengi kwenye system,” Joh alimuambia mtangazaji wa Ice FM, Gami Dee

Na alipoulizwa anamaanisha nini anaposema kuwa na wazee wengi kwenye system Joh alikazia zaidi,”kwasababu dunia inabadilika na vijana ndio wanarun dunia sasa kama mtu wanaendesha vitu katika kimiaka ya nyuma lazima tuchelewe kufika lazima vitu viende kisasa, muziki ni biashara na wasanii wanaweza kuchangia sana pato la taifa kwahiyo wapewe sapoti inavyohitajika.”

Kuhusiana na kauli ya Young Killer kuwa Joh anabebwa Joh alisema, “Sawa ya upuuzi ni kupuizia tu hivyo ukifuata ya wapuuzi nawe utakuwa mpuuzi.”

 

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.