JINSI YA KUTUNZA FURAHA NA UPENDO KATIKA MAHUSIANO YAKO

0

Watu Wengi ambao Wako Kwenye mahusiano Wanalalamika Kuwa Wenzi Wao hawawaoneshi Upendo Kama Ilivyokuwa Siku Za Mwanzo Za Uhusiano Wao,Kuwa katika mahusiano sio adhabu,ni imani yangu kiwa uliingia katika mahusiano yako ukiwa na imani kuwa unaenda kupata furaha na sio karaha.Usjali!kama uko katika uhusiano na unaona furaha na upendo umepungua,ambatana nami hatua kwa hatua katika makala hii natumaini utapata kitu kipya.

Zifuatazo Ni Mbinu Zitakazokusaidia

1. CHEKE NA MPENZI WAKO/UNAE HUSIANA NAE.
Unashangaa!!unaanzaje kucheka na wakati huna furaha,? Umeskia wazungu wana sema SMILE KILLS Sikiliza ndugu yangu tabasamu lako ndio siraha yako kubwa sana katika mahusiano yako.!
Kicheko Ni Mlango Wa Ukaribu, Kama Maneza Kucheka Pamoja Basi Mnaweza Kulia Pamoja, Na hapa Mnaweza Kuaminiana Zaidi Katika Kuwasiliana Hisia Zenu,na kama kuna jambo linawasumbua mnashirikiana kwa pamoja kulitatua mkiwa katika hali ya furaha.

2.KUTIANA MOYO,KUSAIDIANA NA KUPONGEZANA

Kila Mmoja Awe Msaada Na Tegemeo Kwa Mwenzake. Jifunze Kumtia Moyo Na Kumwezesha Mwenzako. Sikiliza Na Kufuatilia Vile mwenzako anavyo jighulisha navyo.!Hapa unaweza kuzidisha kiherehere hata wakati mwingine nenda kazini kwake ukampe ushirikiano huko,yawezekena hata anacho kifanya mwenzi wako wewe hukipendi,lakini ukiwa unafahamu “UKIPENDA BOGA PENDA NA UWA LAKE” hutajiskia vibaya,
Kila Upatapo Nafasi Mpongeze Mbele Za Watu Au Hata Unapokua Nae Peke Yenu. Mjenge Mwenzako Mbele Ya wengine Na Kubali Pongezi Zote Za Mafanikio Yenu Zimwendee Yeye.

3. MGUSE MPENZI WAKO
ANGALIZO;Zinaa ni dhambi!
Nimeona niweke angalizo mapemaa maana sitaki nipate dhambi kwa Mungu wangu ili nikufurahishe wewe! Mguso ninao zungumzia hapa si ule wakule kitandani!La hasha! Hapa na zungu mzia Kushikana mikono,kukumbatiana(Hugs),simple kiss(Mabusu ya kiungwana) na kama imani yako hairuhusu kugusana DADA YANGU NA KAKA YANGU NIKUSHAURI FANYA HARAKA UFUNGE NDOA NA MWENZI WAKO

4.ZUNGUMZA NA MWENZAKO(FUNGUKA)

Kati Ya Vikwazo Vikubwa Katika Ustawi Wa Uhusiano Mengi Hususan Ya Wanandoa Ni Kutokuwepo Kwa Majadiliano. Lazima Wapenzi Wajifunze Kuzungumza Kuhusu Hisia Zao. Kama Vile Maisha Yasivyo Na Ukamilifu, Uhusiano Na Hata Ndoa Pia Hazina Ukamilifu. Mpenzi Wako Hayuko Kamili Na Wala Wewe Pia Siyo Mkamilifu. Jifunze Kuzungumza Na Umpendaye Jinsi Unavyojisikia Na Nini Kinachokusumbua.

5. OMBA MSAMAHA,USISAHAU KUSAMEHE.

Kamwe Tusiache Maumivu Na Machungu Yatawale Uhusiano Wetu. Lazima Tujifunze Kuwasamehe Tuwapendao Na Kujisamehe Sisi Pia. Kutofautiana Katika Uhusiano Kupo Sana, Na Lazima Tuwape Tuwapendao Nafasi Ya Kuelezea Vile Vinavyowaudhi Dhidi Yetu. Kila Hisia Za Mmoja Wetu Zina Umuhimu. Huwezi Kujiona Vile Ulivyo, Mruhusu Mwenzako Akwambie Yanayomuumiza Na Msameheane.Kumbuka hakuma alie mkamilifu nakila mtu anamapungufu yake!
Na Kaka Emma

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.