JINSI YA KUMFANYA MPENZI WAKO AKUPENDE

Wanaume wengi wanajua kutongoza kwa kuzania kuwa tukishakubaliwa basi mapenzi ndo huwa yanaanza papo hapo.. Hahahaha sicheki kwa mazuri ila najaribu kuweka mambo sawa kwa sababu kwa tafiti nlizofanya mahusiano mengi huwa hayadumu na yakidumu sana bas huwa kuna udanganyifu yaaan michepuko lazima ihusike
Hamna wa kumlaumu kwa hili jambo kwa sababu ni uelewa tu unatakiwa…. Si mjanja kwenye haya mambo ila nimejaribu kuelezea sifa tano za kumfanya mpenzi wako akupende

1.ONYESHA DALILI ZA UTU UZIMA
Utu uzima haujagi kwa kuangalia umri wa mtu bali kwa mwenendo halisi wa mtu kwanzia muonekano wa nje hadi wa ndani. Ukiwa na mpenzi wako jaribu kutumia lugha nzuri.. Jitahidi kuchagua maneno ya kutumia ukiwa na mpenzi wako, sio lugha tu bali mavazi nayo huchangia..msome mwenzi wako ni mtu wa Aina gani.. Je ni mtu wa kujirusha? basi nenda na trend.. Je ni mtu wa kujiheshimu? basi jitahid uvae mavazi hayo hayo
Pia Mwanamke hupenda mwanamume mwenye malengo.. Mwanaume anayejua nini Anafanya kwa wakati uliopo na ujao na sio mwanaume muda wote unaangaika kwenye mapenzi

2.ONYESHA MAHABA
Muonyeshee mwenzi wako Mahaba kwa ujumla.. Wanaume hudhani wanawake hupenda vitu vikubwa lakini jaribu kumsoma mwanamke wako hupenda vitu gani au hupenda kufanya nini. Onyesha mahaba kwa mfano; kwa kumpelekea zawadi,kumpelekea maua,.. Ni mifano tu ya kaonyesha kwa sababu sio kila mwanamke hupenda hivyo vitu.
Cha muhimu ni kumfanya ajiskie yeye ni wa muhimu kwako
Mwambie unampenda kwa sauti ya taratibu maskioni mwaka, busu ni lugha nzuri La kuwasilana kwa wapendwa mfano;m’busu kwenye paji La uso kwa ishara ya kuwa unamuamini, m’busu shingoni kwa ishara ya kuwa yeye ni anavutia, m’busu kwenye midomo yake taratibu kwa ishara ya kuwa yeye ni mzuri,.. Nk

3.MUDA WA KUSHINDA NAE
Kumfanya mwanamke wako akukumbuke ni jambo La kujivunia pia kwa mwanaume yoyote ila isizidi kiasi cha kumfanya mwanamke ajisikie kuwa yeye hayupo kwenye ratiba zako za kila siku. Jali muda kwa kumjulia hali angalau asubuhi na joni, tafuta muda wa kushinda nae hata wikiendi ni vizuri kwa mtu mwenye ratiba inayom’bana siku za wiki . ukiwa nae msikilize kwa umakini hata kama anaongea pumba, muangalie machoni wakati wa mazungumzo yenu, msome anapenda stori au mada zipi, chakula kipi anapenda.
Muda ni sehemu nzuri ya watu kujuana kwa undani Kupitia mazungumzo ya maneno na vitendo kwa ujumla, ni sehemu muhimu ya kuwafanya wewe na mpenzi wako mzoeane na ni wakati mzuri wa kujenga historia yenu ya mahusiano

4.MPE SIFA INAPOSTAHILI
wanawake wengi hutumia muda mwingi kwenye urembo wao yani mwili na mavazi,hii yote ni kuwa mrembo mbele yako.msifie mpenzi wako, mfanye ajiskie yeye ni mzuri kwako na hamna mwingine zaidi yake wa kumzidi kwenye mboni zako.
Sio kwenye urembo tu bali hata kwa mwenendo mzima wa harakati zenu za mapenzi. Mwambie jinsi alivyo mwenye busara, mtanashati, kujielewa,mtiifu.
Jambo La kutosahau ni kuwa makini na hayo maneno kwa kutoa hizo sifa kwa wakati na muda unaotakiwa na sio kila muda wewe unasifia tu.. Hapo utaonekana muigizaji

5.MPE MUDA
usijifanye wewe ndo wa kwanza kupenda yani kila mara umemganda mwenzi wako kama kucha….mpe muda mpenzi wako afanye vitu vyake vilivyo na visivyo ndani ya ratiba yake.jambo litakalo kutatiza kwake,jaribu kuzungumza na watu wa karibu wanaowajua ila sio vizuri kumuendea yeye bila kufanya uchunguzi.
Wanawake wengi hupenda kuaminiwa kwa kila jambo alifanyalo na huwa hawapendi wapenzi wao waonyeshe mapungufu hayo.jaribu kuwa mtu unayejiamini kwa chochote kile kiasi cha kwamba huna tatizo kwa muenendo wowote wa kwake.
Usijipe shida kwa sababu hamjaoana na kila mtu anao uhuru wa kufanya anachotaka

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.