JINSI YA KUKABILIANA NA TATIZO LA KUKOSA HISIA ZA TENDO LA NDOA

WIKI iliyopita nilianza kuzungumzia mada yenye kichwa cha habari kilichopo hapo juu, leo nitaendelea pale nilipoishia. Iko hivi, mtu yeyote awe mwanamke au mwanaume mwenye hamu na hisia kubwa za kushiriki ngono kitaalamu huitwa Hypersexuality na yule mwenye kiwango kidogo tunaita Hyposexuality.

Huwa inatokea mtu akawa na hamu sana ya kuhitaji kushiriki ngono, lakini mazingira hayamruhusu au sheria fulanifulani zinambana kutokana na misingi au taratibu mbalimbali, mfano za kidini au kijamii au kimaadili.

 

Basi endapo itatokea atashindwa kujidhibiti au kudhibitiwa na akaipata fursa hiyo, huanza kushiriki kwa fujo bila kuangalia anayemfuatilia na kushiriki naye ni mtu wa aina gani, kwa hiyo wakati mwingine mtu anaweza kujikuta amedumbukia katika dimbwi la ngono bila kujijua alianza vipi kumbe ni kushindwa kudhibiti hali ya hisia zake na hamu.

 

Haja na utashi wa kushiriki tendo la kujamiiana miongoni mwa binadamu husaidia kuimarisha maelewano mazuri endapo wawili hao watakuwa na mawasiliano mazuri.

 

 

Katika hili, endapo mmojawapo kila mara hayupo tayari, yaani hana haja wala utashi wa kushiriki tendo hili, basi mgogoro mkubwa katika mahusiano utatokea na kuharibu umoja uliopo. Mawasiliano mabovu katika mapenzi pia huvunja mahusiano na kusababisha matatizo makubwa kutokana na kutojali nini mwenza wako angependa au kupendelea katika mapenzi. Endapo itatokea mtu hana hamu na hisia za kutosha katika kufanya tendo la ndoa lakini siku zote haridhishwi na tendo linavyofanyika kutoka kwa mpenzi wake, basi tunasema mtu huyo ana njaa na kiu ya mapenzi ambayo haijakamilishwa hivyo yupo hatarini kupata tatizo liitwalo sexual frustration, ambapo anashindwa kumaliza msongo wa mapenzi uliombana.

 

Mtu mwenye dalili hizi kama ni mwanamke huanza kufuatilia vijana wadogo kwani huhisi watu wazima wenzake ndiyo tatizo, kama ni mwanaume kijana huanza kufuatilia wamama watu wazima kwa kuhisi wasichana au wanawake wa rika lake ni tatizo. Kwa wanaume watu wazima na wazee hufuatilia wasichana wadogo, kwa makundi haya ya watu tunasema tayari wameathirika kimapenzi, hawajawahi kuridhishwa hivyo wapo sexually frustrated.

 

MATATIZO YA KISAIKOLOJIA

 

Wanazuoni na wasomi mbalimbali wa hapo kale walishayaona haya tangu hapo awali, mwanazuoni Sigmund Freud alizungumzia libido kuwa ni nguvu kubwa au nishati iliyo ndani ya penzi bila mtu mwenyewe kujifahamu na kujikuta kadumbukia katika mapenzi kwa kumpenda na kuwa na hamu kubwa ya kuwa na ampendaye. Pia mwanazuoni huyo amezungumzia hatua mbalimbali za hamu na hisia za mapenzi na kujamiiana zinavyoanza tangu utotoni.

 

MATATIZO YANAYOATHIRI HAMU NA HISIA ZA TENDO LA NDOA

Matatizo haya yanahusishwa na vichocheo na kemikali mbalimbali za mwilini, kitaalamu tunaita Endogenous Compounds ambavyo tayari tumeshavizungumzia kwa kufupi. Mfano homoni na Neurotransmitters. Vichocheo na kemikali hizi pamoja na kusaidia hamu na hisia za ngono, kwa mwanamke humjenga na kumfanya afike kileleni wakati wa tendo na kabla ya tendo atoe majimaji ya kulainisha uke. Endapo hali hii haitakuwepo, huyu
mwanamke atalalamika uke kuwa mkavu na kupata maumivu wakati wa tendo.

 

MATATIZO KATIKA MFUMO WA HOMONI

Homoni au vichocheo vinavyomfanya mwanamke awe na hamu kubwa ya tendo la ndoa ni Testosterone. Vichocheo hivi huongezeka mara tu mwanamke anapomaliza hedhi yake hadi siku mbili kabla ya kupevusha mayai. Kipindi cha Ovulation ambacho mayai hupevuka Testosterone hupungua na ile hamu kubwa ya tendo la ndoa hupungua. Uwepo wa homoni ya progesterone baada tu ya ovulation husababisha ugumu kidogo kwa mwanamke kufikia kileleni.

 

Kwa mwanamke yeyote alie katika umri wa kuzaa, kiwango cha homoni ya Estrogen huwa juu, hivyo basi, njia yoyote au uwezekano wowote wa kufanya Progesterone ipande, hushusha Estrogen na kusababisha mwanamke awe na uke mkavu, apate maumivu wakati wa tendo la ndoa na kupoteza hamu ya tendo la ndoa, hali hii huwatokea zaidi wanawake waliofikia ukomo wa uzazi. Pamoja na kipindi hiki kuwa ni kipindi cha uzee au utu uzima kwa mwanamke, viwango vya homoni ya Estrogen hushuka, lakini homoni au kichocheo cha Testosterone hupanda sana na kumfanya mama huyu mtu mzima kuwa na hamu sana ya tendo la ndoa lakini uwezo wa kulifanya unapotea kutokana na kukosa majimaji ya kulainisha uke.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.