JINSI HISTORIA INAVYOPINGA MBOWE KUWA MTETEZI WA WANYONGE

Mimi ni muumini wa Historia ya ukombozi, ninafahamu dunia nzima namna nchi zilizohitaji ukombozi namna zilivyopata ukombozi na namna ya viongozi wao waliowakomboa walivyojitokeza kwenye jamii.

Mbowe ndio mfanyabiashara pekee anayejiita mtetezi wa masikini duniani, tangu nimewahi kuifahamu historia ya ukombozi,

Hakujawahi kutokea Duniani labda ahera, Masikini wakatetewa na Tajiri, Haijawahi na Jaitawahi kutokea Mfanya biashara yoyote akapanga kupata hasarfa eti kwa maslahi ya Umma, wafanya biashara wote wanawaza faida, hata mbowe anawaza faida na sasa anatafuta faida kwa gharama yoyote.

Tunamsifia Mandela leo, Mandela hakuwa mfanyabiashara, Mandela hakuwa tajiri, Mandela alichangiwa na masikini wenzake kuikomboa Arika ya Kusini, Mandela hakuwahi Kuikopesha ANC pesa ili iwaondoe Makaburuu, Mandela alifanana na jamii aliyotaka kuikomboa na Mandela alifanikiwa kuikomboa.

Wote tunamsifia Nyerere Hapa Tanzania, Nyerere Hakuwa Mfanyabiashara, mwalimu Hakuwa Tajiri, mwalimu Hakuwahi kuikopesha TANU ili kumuondoa MKOLONI, nyerere alichangiwa na masikini wenzake, aliombewa na walalhoi wenzake na alilindwa na mafukara wenzake.

Mifano ni mingi, hivyo hivyo kwa Samora Machel, Kwame Nkuruma, Milton Obote, Robert Mugabe, Kamuzu Banda, Dkt Martin Lutherking, Mahatma Gandh, Mao Zedong, AmilicaCabra na wengineo wote, KAMWE KUNGURU WASIOFANANA HAWAWEZI KURUKA PAMOJA.
Nitaendelea kuwafundisha mengi ninayoyajua kuhusu MBOWE NA CHADEMA kwa kadri itakavyowezekana.

Jamii Forums

 

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.