Jeshi la Uganda lasema halina mpango wa kuingia Kenya

Jeshi la Uganda Jeshi la Uganda la UPDF limekanusha taarifa kuwa liko tayari kuingia nchini Kenya kusaidia kudhibiti hali ya usalama nchini humo baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa wiki iliyopita.

Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi, huku mpinzani wake mkuu Raila Odinga akiyapinga matokeo hayo.

Waziri wa mawasiliano nchini humo Frank Tumwebaze amesema jeshi la Uganda haliwezi kutumwa nje kushiriki operesheni ya kijeshi kisiri.

Msemaji wa jeshi la Uganda Richard Karemire, kupitia taarifa, amesema Kenya ni nchi huru na usalama wake umo chini ya serikali ya nchi hiyo.

Aidha, amesema Uganda haijapokea ombi kutoka kwa Kenya kutuma majeshi yake nchini humo au kuomba usaidizi.

Mwandishi wa BBC Siraj Kalyango anaarifu zaidi.

BBC

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.