Jengo la Yanga kupigwa mnada Agosti 19

Mahakama yaamuru Jengo la klabu ya Yanga lililopo maeneo ya Jangwani kuuzwa kwa mnada Agosti 19 baada ya kudaiwa kodi ya ardhi ya zaidi ya shilingi milioni 300.

Hata hivyo uongozi wa klabu ya Yanga umeeleza kushtushwa na hatua ya serikali kutaka kulipiga mnada jengo hilo ambalo ni makao ya klabu na kuahidi kufanya kila linalowezekana kunusuru hali hiyo.

Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Charles Boniface Mkwasa
Amesema kuwa “Ni kweli tuna deni kubwa tunadaiwa la ardhi, lakini tayari tulishakubaliana namna ya kulilipa kupitia mapato yetu ya milangoni” – Mkwasa

Boniface Mkwasa ameongeza kuwa “Kodi tunayopaswa kulipa kwa mwaka ni shilingi milioni 59, na hatujalipa miaka mingi kwahiyo tunadaiwa pesa nyingi”.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.