Je? Wajua Madhara Yatokanayo Na Matumizi Ya Lipstick Kwa Muda Mrefu

0

Kila siku mamilioni ya wanawake hujipaka lipstick bila kufikiria hata kidogo – wanachojali wao ni muonekano na urembo wao.

Kikubwa wasichofahamu ni kwamba baadhi ya lipsticks zimegunduliwa kuwa na madini ya LEAD ambayo yanaweza kusababisha matatizo katika uwezo wako wa kujifunza, lugha na tabia kwa ujumla. Lead inaweza kukusababishia matatizo ya mfumo wa fahamu hata kiasi kidogo tu kiingiapo kwenye damu.

Je Lead inafanya kazi gani kwenye Lipstick?

Sio Lipstick zote zinakiambato cha Lead, lakini katika utafiti uliofanyika hivi karibuni inaonyesha kuwa viwanda vingi vinapendelea kuchanganya madini haya katika siku za hivi karibuni. 2007 katika utafiti ulioitwa — “A Poison Kiss” – ulioweza kuonyesha 61% ya lipstick 33 zilizofanyiwa utafiti zilikuwa na kiasi cha Lead kuanzia 0.03ppm mpaka 0.65 ppm.

Kiujumla hakuna kiasi ambacho tunaweza sema kuwa hiki ni salama cha Lead katika mwili wa binadamu. Hata FDA ya Marekani haitilii shaka sana suala la uwepo wa madini ya lead kwenye Lipstick. Hakuna lipstick ambayo imeainishwa moja kwa moja kuwa ina kiambato cha lead na watengenezaji wake.

Kiasi cha lead huwa kidogo, lakini uwepo wake ndio unaotilia shaka kuhusiana na suala la kumezwa (ingestion) na kupenya (absorption) kupitia ngozi ndivyo vinavyoleta wasiwasi katika swala la usalama kuhusiana na bidhaa za vipodozi kwa wanawake.

Utafiti uliofanywa na FDA ya Marekani mwaka 2010 uliweza kutambua madini ya Lead katika aina 400 za lipsticks zilizofanyiwa tafiti na zilionyesha kuwa na kiasi cha lead kuanzia 0.9 ppm mpaka 3.06 ppm. Pia tutambue kuwa madini ya Lead sio madini pekee ambayo ni hatari kutumika kwenye lipsticks.

Utafiti uliofanywa pia na chuo kikuu cha Califonia Marekani katika aina 24 za lipsticks ziliweza kugundua uwepo wa madini hatari ya chromium, cadmium, manganese, aluminium na lead. FDA inasema kuwa kiasi cha madini ya Lead katika lipstick ambacho nia na madhumuni yake ni kwa ajili ya kupaka nje ya mwili sio hatari wasiwasi ni pale unaporamba lips zako na kuyafanya madini haya kuingia ndani ya mwili mpaka kwenye damu.

Ni ukweli usiofichika kuwa upakaji wa Lipstick mara moja kwa siku hauwezi kukuletea madhara yeyote na sio lipsticks zote zina madini haya hatari niliyoyataja hapo juu. (Na pia bei ya lipsticks iwe kubwa au ndogo sio kigezo cha kiasi cha Lead kinachopatikana ndani yake.)

Tatizo linakuja pale wamapojipaka lipstick mara mbili (2) mpaka 14 kwa siku kutokana na utafiti ulifanyika katika chuo kikuu cha California. Matokeo yanaonyesha kuwa wanawake hawa wanameza au wanapenyeza zaidi ya gramu 87 (87gm) kwa siku, hivyo kama watatumia kwa muda mrefu wana hatari kubwa ya kupata madhara yatokanayo na madini hatari ya lead.

Changamoto ni kwamba ukiyatoa madini ya Aluminium, madini hayo mengine vaingia kama rangi (pigments) na msingi ya vitu (base materials) vingine vinavyotumika kutengeneza lipsticks. Kitu hichi kinawafanya watengenezaji wa bidhaa hizi kutohitajika kuyaainisha madini haya kama viambato katika lebo zao.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.