JE UNAFAHAMU KUWA WOGA WAKO KTK KUTHUBUTU NI SILAHA YA SHETANI YA KUKUANGAMIZA.?

0

Hali mbaya ya kimaisha,uchumi mbovu,afya mbovu au umaskini kwa ujumla wake ni Mapenzi ya shetani kwa Mwanadamu.Unajua Shetani anafahamu fika kuwa Mungu alivyo muumba mwanadamu alimpa mamlaka ya kutawala na kumiliki vitu vyote vilivyo ndani ya dunia,lakini haikuishia kwenye kupewa tu umiliki pia Mungu amempa mwanadamu uwezo na akili kubwa ya kuimili na kuitawala dunia.Shetani baada ya kuona Mwanadamu amepewa uwezo mkubwa na Mungu yeye akaja na virus wake anaitwa WOGA,Hapa alikuwa ameweza kabisa kuharibu ule uwezo,akili na mamlaka ya kumiliki ulimwengu alio pewa mwandamu na Mungu.

Kaka na Dada zangu manao soma makala hii nikukuhakikishie tu kuwa hali yoyote mbaya,shida zozote na umaskini wowote ambao uko nao wewe au jirani yako chanzo kikubwa ni WOGA WA KUTHUBUTU.Sijui kama unanielewa vizuri!IKO HIVI katika makala iliyo pita nilifafanua namna ambavyo unaweza kutambua kipaji chako,sasa basi kama umewweza kutambua kipaji chako na kipaji hiki kimetoka kwa Mungu,na kumbuka Mungualikupa kipaji hiki au uwezo huo uweze Kutengeneza maisha mazuri kupiti hicho,lakini kutoka na kuwa ulivyo zaliwa shetani alikutia WOGA WA KUTHUBUTU na ndiyo Maana mpaka leo hii unaogoapa kutumia uwezo ulokuwa nao kukutengenezea kipato chako.WOGA ni roho,ni kweli haionekani lakini inaona,inasikia na inaongea pia,hivyo basi inahusika sana ktk kukusahuri kufanya Maamuzi ambayo yana zidi kukuingiza ktk Umaskini,Ndiyo maana kila unapotaka kujaribu kufanya Jambo ambalo ni la kimaendeleo WOGA unaanza kuja kukupa ushauri kwenye mawazo yako ustaskia “usijaribu kufanya hicho kitu hakita kupafaida yoyote” zaidi anazidi kukufanya uwaze zaodi upande wa hasara kuliko faida,mwisho wa siku hufanyi na unafata mawazo ya rafiki yako WOGA ambaye hakutakii mema siku zote.

WOGA unatabia ya kujifanya nirafiki sana na wewe,Woga utakupa hadi Mifano ya watu walio shindwa kufanikiwa katika Jambo ambalo wewe pia unataka kujaribu kulifanya bila kukuonyesha ni wapi alikosea,hata siku moja rafiki huyu hawezi kukupa Mifano ya waliofanikiwa kwa kupitia jambo hilo hilona kwakuwa wewe umeshikiwa ufahamu na rafiki Woga hautawaza upande Mwingine wa faida na mwisho wasiku unazidi kuwa na hali mbaya ya umaskini.

Wahenga wakikwambia “woga wako ndiyo umaskini wako” Rafikiyo WOGA bila kupoteza muda nae anakuna na kukwambia “Wenye viherehere ndio wanakufaga Mapema,kuwa na subira” sasa na wewe ulivyo na mapenzi ya dhati na rafiki yako unaendelea kumwaini,unaonsema acha wenzako watangulie kama chambo,undhani wataharibikiwa kumbe ndo wanazidi kufanikiwa unabaki kusema “TULIKJWA NAE KIJIWENI HUYU,TENA MIMI NINA UWEZO ZAIDI YAKE”

Kataa WOGA kwa nguvu na akili zako zote,amini unachotaka kufanya ndiyo haswa Mungu alikuweka hapa duniani kukifanya iliuweze kutawala na kumiliki dunia na kwakuwa Mungu anakuwazia mafanikio lazima utafanikiwa tu.

Na KAKA EMMA

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.