HEKIMA ZA BABU KWA WASICHANA

0

Mambo vipi watu Wangu wa Nguvu.?Natuamini mko Pouwa Kabisa,Upande wangu Mimi mtani wako wa hiari sina tatizo lolote,Namshukuru Allah kwa kuendelea Kunipa Afya njema.

Basi leo sina maneno meengi zaidi ya kukuletea moja kwa moja hekima za Babu yangu ambae ametaka kuzungumza na Mabinti zake juu ya namna ambavyo wanaeweza kuenenda hata katika kupata Mume wa ndoa,SONGA NAE

UJUMBE KWA MABINTI WOTE
1. Mwanaume atakaekutambulisha kwa wazazi wake na
si kwa rafiki zake pekee huyo ndiye mwenye mwelekeo
wa kufanya maisha na wewe.
2. Usitizame gari wala pesa nyingi ukadhani ndio kipimo
cha utajiri wa mwanaume, ndoto na maono yake yenye
tija ndio muelekeo mzuri wa utajiri wa mwanaume.
3. Ni wazi kwamba mwanaume anaweza akakupa talaka
au kukufukuza kwake, ila elimu, ujuzi na kipaji hakiwezi
kukupa talaka. Hivyo basi focus katika kupata elimu na
ujuzi kabla hujampata mwanaume wako.
4. Usikubali ngono ikufanye kuwa mama kabla ya ndoa
kukufanya kuwa mke. Tangulia kwanza kuwa mke ndipo
uwe mama.
5. Wanaume bora sio vigumu kuwapata, ila ni vigumu
kuwavutia. Hivyo basi kama unataka mwanaume bora
jiandae kumvutia. Si kumvutia kimapenzi! La hasha
binti yangu..namaanisha kuwa na tabia na siha njema
anayokufunza mama yako.
6. Matokeo ya kuwadharau wanaume walio bora na
kujichanganya na wanaume matapeli ni kwamba
utakuja kuchanganyikiwa, hasira na visasi pale
utakapoona wale wanaume bora uliowadharau wanaoa
wanawake ambao nao uliwaona kama sio wazuri kama
wewe.
7. Kama utamuuliza Mungu ni nini kanuni ya uchumba
ni rahisi tu; Kama huyo Mwanaume hana Mungu, basi
hastahili kuwa na wewe.
8. Bibi yako enzi za ujana wake alikuwa mzuri kweli,
sasa nakupa agizo hili, kila utembeapo tembea na
picha ya bibi yako katika pochi yako. Ili kila
utakapoifungua pochi picha itakukumbusha kwamba
uzuri ni wa muda tu, ila tabia, hekima na busara
zinadumu milele.
9. Jipende na ujitunze, wewe ni hekalu la mwenyezi
Mungu, Mungu hatapenda kuona hekalu lake
likichafuliwa.
10. Hakuna mpumbavu mkubwa kama mwanamke
ambae anamdharau mwanaume kwa sababu ya hali
yake ya kiuchumi aliyonayo kwa wakati huo.
FIKIRIA CHUKUA HATUA

***********Na KAKA EMMA************

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.