HATUA TATU(3) MUHIMU ZITAKAZO KUWEZESHA KUISHI BILA MSONGO

0

Mwanadamu ameumbwa na mahitaji Mengi sana,kama vile chakula,malazi,mavazi bila kusahau mahitaji mengine kama Elimu na kupenda na kupendwa,yote haya kwa ujumla wake ndio yanaleta maana halisi ya Maisha ya Mwanadamu.Mwanadamu huyu ili aweze kutimiza Mahitaji haya anahitaji kuwa na Amani ndani ya nafsi lakini pia akili iliyo tulia.Kitu kingine cha kufahamu ni kwamba Mwanaadamu huyu katika Utekelezaji wa Majukumu yake ya kupata mahitaji yake si Kwamba yote yanakwenda kama alivyo panga!hapana!wakati Mwingine hutokea  kupata matokeo tofauti na matarajio yake,na hapa ndipo tunaona mwanadamu huyu akiingia kwenye dimbwi la mawazo,anakosa amani,huzuni na akili yake inashindwa kutulia kufanya maamuzi yalio sahihi au kwa lugha ya pamoja tunasema mwanadamu huyu amepata msomgo wa mawazo.
Kwakuwa Wanadamu wameumbwa tofauti,kuna wale ambao wanaweza kupambana na hali hiyo ya Msongo wa Mawazo na kutoka kwa haraka na kisha kuendelea na ratiba zao za kila siku bila shida yoyote na wapo wale ambao wao hawawezi kupambana na hii hali hivyo kuwafanya wazidi kuharibikiwa zaidi.Basi ktk Makala hii nimejaribu kuelezea mambo makuu tatu ambayo ni naamini ukiyazingatia unaweza ukaishi maisha ya furaha bila kuwa na msongo wa mawazo.

1. YATAMBUE MAMBO YOTE YANAYO KUFANYA UWE NA MSONGO WA MAWAZO
Unaweza kujiuliza labda ni kwanini nianze kukumbuka na kuvitambua vitu vinavyo nifanya nikose amani,Lakini nikukumbushe ule usemi unaosema MBWA UKIMJUA JINA HAKUSUMBUI inawezekana kabisa unapata msongo wa mawazo kutoka na sababu moja hiyo hiyo na kila siku umekuwa ukirudia kosa lilelile linakufanya upate msongo wa mawazo,kitu ambacho kingekuwaa tayari kimepata ufumbuzi kama ungekuwa umekwisha kukitambua.Unachotakiwa kufanya sasa nikuchukuwa kuram na karatasi,kisha orodhesha yale yote yanayokufanya upate msongo wa mawazo.

     2. KUBALI MATOKEO
Baada ya kutambua Mambo yote yanayo kisababishia msongo wa mawazo,hatua inayofuta ni kukubali kuwa ulicho orodhesha au jambo lingine lolote litakalo tokea ndiyo sababu kubwa ya ww kuwa na Msongo wa mawazo,usibishane na hisia zako,wala usijaribu kiziongopea hisia zako kuwa kunaweza kukawa na Muujiza wowote wa kubadili kilichotokea.Kama ulikuwa hufahamu basi hili ndio eneo ambalo wengi tunatofautiana ktk Muda wa kubeba msongo wa mawazo,iko hivi ndugu yangu unapokubaliana na matokeo mapema ndio inakupa muda mzuri wa akili kutulia na kuanza kufanya maamuzi sahihi,lakini utakapo kosea na kuanza kujilaumu,nakutaka kuziaminisha hisia zako kuwa kulikuwa na njia nyingine ungeweza kufanya usipate hill tatizo lililopelekea kupata masongo wa mawazo ndugu utachelewa kupona na mwisho msongo huo wa mawazo unaweza kukufanya ufanye jambo ambalo utalijutia maisha.Hivyo basi nakushauri kukubaliana na hali hiyo kwa haraka.Usisahau kuwa jambo likitokea kwako ni lakwako wala si lamtu mwingine.

3.USIISHI MAISHA YA JANA,ISHI MAISHA YA LEO.
Kuna maneno yana sema “Siku ya jana haijapotea,kama utawekeza sana siku ya leo” Inapokuja kwenye msongo wa mawazo watu wengi wamezidi kuumizwa na mawazo hayo kwasababu moja ya kutafakari kile walichopoteza siku ya jana na kusahau kuwa kunakikubwa sana kipo mbele yao kinawasubiria!Unapopatwa na tatizo usipoteze Muda mwingi kwenye kujilaumu au kuwa na wasiwasi na uwezo wako,unachotakiwa kufanya ni kutulia,vutapumzi nyingi,angalia ulikosea wapi,kubali makosa yako,tafuta njia ya kurekebisha makosa yako,kisha songa mbele.
Ni imani yangu Makala hii itakuwa imekusaidia kwa sehemu na kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nami.Usisahau kuacha maoni.!

Na Kaka Emma

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.