Harmonize Afunguka Kuhusu Kuhama WCB

Msanii wa muziki wa Bongo Flava kutoka label ya WCB, Harmonize amejibu iwepo anaweza kuondoka katika label hiyo.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Shulula’ ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa hawezi kufanya hivyo kwa sasa.

“Hapana kwa sababu unapozungumzia Harmonize inaizungumzia WCB, so bila WCB hakuna Harmonize, yaani kama baba kama mama” amesema Harmonize.

Alipoulizwa ni msanii yupi anamkubali katika label hiyo alijibu, “ndani ya WCB nawakubali wote kwa sababu kikubwa kila msanii unayemuona pale hajaja kwa bahati, kila mtu ana kipaji japokuwa wanatofautiana”.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.