HADITHI:S1Ep5b CHEKA NA KAKA EMMA(SCHOOL COMMEDY)

0

Mwl babu akiwa amesubiri karibu masaa matatu bila mafanikio yoyote,Emma alishtuka kutoka usingizini akauliza “mwl babu kwani baba kesha kuja?” wakati huohuo ndiyo na mwl babu alikuwa anajaribu kuendelea kumpigia simu kwa mara ya mwisho na kukuta hali ni ileile ya simu kuita bila kupokelewa “baba yako mpaka sasa hajafika na nikimpigia hapokei sijui anampango gani” Emma alitabasamu kwa kuwa alikuwa anajua tabia za baba yake “mwl babu nilikwambia huyu mzee ni msumbufu kamajina lake labda umpigie mama” mwl babu alivoona Emma anamcheka na nikwafaida yake alikasirika sana akaona sasa njia nzuri ya kumaliza lile tatizo ni kumpeleka Emma nyumbani kwao yeye mwenyewe “we mwanaharamu endelea tu kucheka hapo nitakupeleka kwenu mimi mwenyewe na bakora juu, baba yako si anajifanya kichwa ngumu” Emma aliposikia habari za kupelekwa kwao alifurahi sana,si kwasababu atarudi mapema nyumbani kabla ya wenzake lakini ni kwasababu atapanda pikipiki ya mwl babu “mwl babu hilo ni wazo zuri,mi ningeona ni bora twende hata sasa hivi nikapumzike maana kichwa kinaniuma kweli”
Baada ya kusubiri kwa muda mrefu ikabidi mwl babu achukue mkoba wake kisha akamshika mkono Emma wakatoka nje ya ofisi wakaifunga nakuanza safari ya kuelekea nyumba kwa kina Emma “mmmmmh…!!!prince aliguna baada ya kuona wameanza safari bila hata ya pikipiki ikabidi aulize “mwl mbona hatuendi na pikipiki yako?” mwl babu alivo sikia hivyo hasira zote alizo kuwa nazo ziliisha akaanza kucheka mwenyewe kwakuwa aligundua sababu ya Emma kufurahia kupelekwa nyumbani “pole sana kijana wangu tutatembea kwa miguu mpaka kwenu” Emma alihuzunika sana, akaanza kuona safari haifai tena,”mwl lakini kwetu mbali ujue,we huoni mimi kila siku nachelewa kuwahi namba,ungekodi hata boda boda, kama wewe huna hela tukifika nyumbani mama atalipia” mwl babu baada ya kusikia Emma anasema wakodi bodaboda mama yake atalipia alizidi kucheka “hahahahah..!!we mtoto kweli taahira,pesa ya mlinzi tu mama yako hajawahi kulipa hata siku moja tangu uanze lakwanza,itakuwa bodaboda” Emma hakuwa na lakujibu. Waliendelea na safari bila kuongea lolote kwa muda mrefu kidogo kila mtu akiwa anawaza jambo lake kichwani,Emma alisimama kwa ghafla na kumuuliza mwl babu “eti mwalimu yale majina yalio kuwa pale kwenye meza yako ni vepee,maana jina langu pia lipo???” mwl babu aliona kuna haja ya kumjibu kwakuwa yeye asinge weza kulipa hizo pesa za mlinzi naistoshe wanazidi kuchelewa “we mshenzi usinisumbue na maswali yako ya kipuuzi,ongoza safari twende” Emam alivoona mwl babu kakasirika ikabidi acheke “hahahahahaha..!!lakini mwl kuuliza si ujinga” mwl babu alizidi kukasirika ,akashika mabega ya Emma nakuanza kumtikisa kama maji kwenye dumu “we mshenzi nita kuumiza ujue hebu ongoza safari” baada ya kutikiswa Emma ndo akazidi kuangua kicheko kana kwamba mwl babu alikuwa akimtekenya “hahahahahahahaha…!!we babu vepeee bwana ??twende wapi sasa nawakati tushafika au hupajui nyumbani kwetu”

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.