Fid Q Awataja Mapruducer Wa 3 Wenye Uwezo Wa Kufanya Mixing Na Mastering Bongo

Q amewataja watayarishaji wa muziki Bongo wanaofanya mastering nzuri ambao wasanii wanapaswa kwenda kufanya nao kazi ili wapate nyimbo zenye ubora mkubwa.

Rapper huyo amekiambia kipindi cha Dj Show kuwa maproducer wengi wa hapa nchini hawana uwezo wa kufanya mixing na mastering ndio maana nyimbo nyingi za wasanii zimekuwa siyo nzuri na zimekosa ubora.

“Bongo hii mtu ambaye anaweza akafanya mastering kama anataka kufanya joint ya kimataifa ni producer P-Funk Majani, kuna wengine Marco Chali, Hermy B. Hao ndio maproducer ambao wanaweza wakafanya mastering na ngoma ikawa na kiwango cha kimataifa,” amesema Fid.

“Wasanii wengi wana ngoma nzuri lakini unakuta mixing mbaya na mastering hazijafanyiwa kabisa. Sometimes ukikuta ngoma ya msanii ambayo imefanyiwa mastering vizuri hata kama ni muziki ambao wewe haupendi au hujawahi kuusikia still unaweza ukakuvutia kwa namna moja au nyingine kuusikiliza kutokana na quality ya muziki wenyewe,” ameongeza.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.