Everton Timu Ya Kuogopwa Msimu Huu – Phil Neville

Nahodha wazamani wa Everton, Phil Neville amesema klabu hiyo nimiongoni mwa timu zinazopaswa kuchungwa sana msimu huu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza.

Phil Neville amesema kurejea kwa Rooney katika klabu ya Everton nimoja ya sababu ya kufaniki wa katika dirisha hili la usajili

Neville anaamini kurejea kwa mchezaji, Wayne Rooney na namna Toffees ilivyo imarika katika usajili wa msimu huu kunaonyesha ubora wake na upinzani mkubwa utakao onyeshwa baada ya kuanza kwa ligi.

Mchezaji huyo ameongeza kuwa wenyeji hao wa Goodson Park wameonyesha nia ya kupanda katika msimamo wa ligi kama walivyofanikiwa Spurs huku akiamini kama dirisha la usajili lingefungwa leo basi Everton imefanya usajili bora.

Everton imekuwa makini katika dirisha hili la usajili msimu huu ikiwa chini ya Meneja wake, Ronald Koeman imemsajili mlindalango wa Sunderland, Jordan Pickford, kiungo wa Ajax, Davy Klaassen, beki wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Burnley, Michael Keane pamoja na beki mwingine wa Southampton, Cuco Martina.

Lakini pia klabu hiyo imefanikiwa kumuuza mchezaji Romelu Lukaku kwa dau nono la pauni milioni 75 kwenda United, Sandro Ramirez kwenda Malaga na kumuingiza kikosini Rooney akitokea Manchester United

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.