VIDEO: DELE ALI ASHINDWA KUFANYA ALICHOFANYA RONALDO

0

Goli la faulu alilofunga Mreno Christiano Ronaldo dhidi ya Portsmouth mwaka 2008 linaaminika ni goli bora kuwahi kutokea katika historia ya soka la uingereza, ambapo staa huyo aliuelekeza mpira huo wa faulu katika pembe(ya kulia) ya juu ya goli na kumuacha kipa wa ‘Pompeys’ bila ya chaguo zaidi ya kusimama pahali alipokuwa.

Ukitaka kuamini Ronaldo aliipiga faulo hiyo Kiustadi,  #Goal Recreated ya  BT sport ilimpatia Dele Ali nafasi ya kupiga faulo nne(4) lakini alishindwa kufunga goli la namna hiyo katika faulo zote nne.

Staa mwenzake Kyle Walker alisikika akisema anataka afurahie endapo Dele Ali atafunga goli kama hilo, lakini Ali mwenyewe alisema “Sahau kuhusu kunifurahia, siwezi kufunga goli kama hilo.”

Staa huyo wa uingereza anaekuja kwa kasi, faulo yake ya kwanza kuipiga iligonga ukuta wa sanamu za walinzi, kisha alipiga mwamba wa juu mara mbili na kupaza juu mara moja kukamilisha nafasi nne hizo alizopewa.

Kabla hata hajaanza kupiga faulo ya kwanza Deli Ali alisema kwamba wanaweza wakashinda siku nzima wakijaribu kufnga namna hiyo.

“Jamani naona tunaweza kushinda hapa kutwa na tusiweze kufunga goli la namna hii”

Alisikika akisema Dale Ali.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.