Cristiano Ronaldo Akaribia Kuitwa Baba Kwa Mara Nyingine Tena…!!!!

Mchezaji bora wa dunia kutoka Real Madrid, Cristiano Ronaldo amethibitisha kuwa muda si mrefu atakuwa anaitwa baba kwa mara nyingine tena.

Hivi karibuni zilisambaa tetesi za mpenzi wa mchezaji huyo ambaye ni mwanamitindo, Georgina Rodriguez kuwa na ujauzito wa miezi mitano.

Akiongea na gazeti la Hispania la El Mundo, mchezaji huyo aliulizwa kama anafurahia kuwa na mtoto mwingine ambaye yupo njiani, Ronaldo alijibu, “Yes, very much.”

Kwa sasa mchezaji huyo ana watoto watatu akiwemo Cristiano Ronaldo Jr mwenye miaka saba na mapacha wake aliwapata hvi karibuni Eva Maria na Mateo.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.