CHUKUA HII: JINSI YA KUSAFISHA USO WAKO

0

Hakikisha unatenga walau dakika kumi kila siku asubuhi kwa ajili ya usafi wa ngozi ya uso wako.

Unapoamka asubuhi, safisha uso wako kwa maji ya uvuguvugu na utumie sabuni uliyoshauriwa na mtaalamu au unayotumia kuoshea uso wako mara kwa mara.

Pia epuka kutumia sabuni ya kipande, kwani hijatengenezwa maalumu kwa ajili ya uso na huweza kufanya ngozi ya uso kukomaa na kupauka.

Ni kawaida ngozi ya uso kuonekana iliyochoka hasa inapofika jioni, baada ya mizunguko ya kutwa nzima, hivyo basi ili kuhakikisha unakuwa na ngozi ya uso iliyochangamka wakati wote kwa kuiosha, lakini unatakiwa kuwa makini zaidi katika hili.

Hakikisha unaosha uso wako vizuri wakati unaoga au wakati unanawa bafuni au popote panapofaa baada ya mizunguko yako ya kutwa.

Tumia kitambaa au kitu laini kusafisha uso wako kwani husaidia kuondoa uchafu ulioganda usoni.Zoezi hili linatakiwa kufanywa kwa uangalifu ili kuhakikisha hauchubui wala kujiumiza ngozi, hakikisha ngozi yako haiwi na magamba ya aina yoyote kwani lengo la kutunza ngozi ni iwe na unyevunyevu na ya  kuvutia.

Unaweza kutumia ‘tona’ kusafisha uso wako kwani husaidia kuondoa uchafu ulioganda.

Jambo kubwa la kuzingatia ni kuhakikisha haulali na vipodozi ulivyopaka asubuhi au mchana, kwani husababisha ngozi yako kukosa hewa.

Kwa matokeo mazuri ya afya ya ngozi ya uso wako, zingatia usafi, kunywa maji mengi na kula mboga za majani na matunda kwa wingi.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.