BONGO FREVA INAHITAJI MUUNGANIKO WA JIDE NA MWANA FA TENA

0

 

Watu ambao muunganiko wao umeunganishwa kutokea mbinguni iwe marafiki, wapenzi au wanandoa basi matokeo ya kile walichounganishiwa huwa na msisimko na ladha ya kipekee. Kama ni ndoa huwa na furaha na mmiminiko wa Baraka. Kama ni muziki basi huwa ni muziki ambao si rahisi ladha yake kuisha.

Alikufa Kwa Ngoma, Hawajui, Sikiliza, Msiache Kuongea,ukisikiliza hizi nyimbo pasi na shaka utakubaliana kuwa sio tu ni moja kati ya nyimbo kali kuwahi kutokea kwenye muziki wetu ila ni moja kati ya nyimbo bora kabisa za kushirikiana katika muziki wa Bongo Flava.

Mara zote ambapo sauti ya mwanadada Lady Jaydee na flow kali za Mwana FA zilipokutana, matokeo yake yalikuwa ni ngoma kali ambazo hata leo ukipata muda wa kusikiliza bado zina ladha ile ile kama zimetoka jana.

Naamini sio peke yangu ninayetamani kusikia watu hawa wakifanya kazi tena, muziki na spika za radio zimemisi na mashabiki kwa ujumla wanatamani kuona na kusikia FA na Jide wakirindima kwenye stations za radio na TV mbalimbali. Kwanini usitamani hasa ukikumbuka ni nadra kwa sasa kutokea chemistry ya aina yake na yenye kusisimua kama ya commando na Binamu!

Ukirudisha miaka kumi nyuma pengine ingekuwa ngumu mtu angekuambia Mwana FA na Jide wanaweza kugombana, unaamini vipi kwa jinsi walivyoshibana kiasi cha Mwana FA kusimamia ndoa ya Jaydee,lakini ilitokea miaka michache nyuma FA na JIDE walitofautiana vikali sana,sijui nini kiliwafikisha huko,lakini hawapo sawa na sio rahisi kwa wao kufanya kazi kwa sasa!

My sister Jide na big bro FA, mashabiki tumemis kuwasikia pamoja,naamini hakuna linaloshindikana chini ya jua. Fanyeni kwa maslahi ya Bongo Flava na mashabiki wake, kwa ajili ya wasanii wachanga ambao kwa nyie kuwa sawa si tu kutawafanya waachane na ugomvi usio na faida kwenye muziki ila mtakuwa mmeonyesha mfano bora na wa kuigwa.

Chemistry yenu ni hela pia,kwanini mziache hela ambazo zingeweza kupatikana kwa nyie kufanya kazi pamoja kisa tu mna ugomvi? Mi sijui mnawezaje kumaliza ila natamani kusikia sauti zenu zikisikika kwa pamoja.

Eliezer Gibson ”Green City Native”

Insta@gibson_elly

Fb Eliezer Gibson

 

 

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.