Banda Aacha Neno Kwa Simba

Hatimaye beki wa Taifa Stars, Abdi Banda ameondoka leo kuelekea nchini Afrika Kusini kwenda kusakata soka la kulipwa katika timu yake mpya ya Baroka FC ambayo amesaini kandarasi ya miaka mitatu
Beki huyo amekwea ‘Pipa’ licha kutopata barua ya kuondoka katika klabu yake ya Simba alipokuwa anachezea msimu uliyopita, mbali na hilo Banda ameshauri wachezaji wenzake ambao wanatamani kupata nafasi ya kucheza nje ya nchi wasiangalie nyuma pindi wanapokuwa wamepata nafasi hizo.
“Wachezaji wajitume na wanatakiwa kuwa makini na nafasi zinapotokea nafasi za kutoka kwenda kucheza nje ya nchi, wasiangalie nyuma wazitumie nafasi hizo. Tunahitaji timu ya taifa nzuri, bila wachezaji wengi kucheza nje ya Tanzania hatuwezi kupata timu nzuri ya taifa na kikubwa ni kuongeza juhudi na kufanya mipango ili wachezaji wengi tucheze nje ya nchi”, amesema Banda.
Banda tayari alishasaini mkataba wa kujiunga na klabu hiyo wakati akiwa kwenye michuano ya COSAFA Cup 2017 mashindano ambayo yamemalizika Afrika Kusini huku Tanzania ikishika nafasi ya tatu.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.