Baby Madaha Ni Free Mason…?

Mwanamuziki na muigizaji kutoka Bongo, Baby Madaha.

MWANAMUZIKI ambaye pia ni muigizaji kutoka Bongo, Baby Madaha ametoboa juu ya namba 666 ambayo anaitumia kwa sasa ikiwemo kwenye mitandao ya kijamii.

Akichonga na Star Mix, Baby Madaha alisema kuweka namba hiyo mbele ya jina lake inamaanisha haki, uwazi na usawa na si alama ya kishetani kama wengi wanavyofikiria.

“Watu wengi wanaamini namba 666 inamaanisha mambo ya kishetani, lakini ninaamini namba hii inamaanisha haki, usawa na uwazi, basi,” alisema Baby Madaha.

Alipobanwa juu ya vitabu vya Mungu kuizungumzia namba hiyo kuhusika na masuala ya kishetani alisema kuwa hana la kuongeza kwani anachoelewa ndicho anachomaanisha anapoitumia namba hiyo

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.