Baada Ya Kufanya Collabo Na 2 pac Sasa Chid Benz Afanya Na Jay Z

Mwishoni mwa wiki iliyopita Chid Benz alishangaza watu kwa kudai amefanya kolabo na Tupac ambaye kwa sasa ni marehemu. Katika kutolea ufafanuzi kauli yake hiyo Chid kaibua lingine la kuwa na kolabo na Jay Z.

Licha ya kuonekana kuzungumza katika hali ya utani kiasi katika mahojiano na FNL ya EATV, Chid alisema kauli ya mwanzo aliitoa kama utani ingawa watu wameichukulia tofauti na kuelezea katika uhalisia wa sasa ana kolabo na Jay Z, je watu wataichukulia kama mwanzo?, alihoji.

“Na hiyo ninayo CD home ipo kwa mama Benz nimeuchuna, nina kolabo na Jay Z nimefanya naye, Beyonce kapiga chorus lakini nataka nimtoe nimuweke pale hata Linah. So watu wanaosema nimelewa au natumia madawa now nina kolabo na Jay Z, ile nilikua natania tu,” amesema Chid Benz.

Katika hatua nyingine Chid alieleza kutofurahishwa na tweet ya msanii Madee kipindi ambacho suala lake lina-trend katika mitandao ya kijamii.

“Madee amejifanya kuposti pale ndio maana mimi sivuti hata sigara, sasa unaweza ukawa huvuti sigara lakini tukawa tunajua wewe ni mmbeya, mnafiki kwa sababu ndio tabia yake. Anaonyesha watu kuna kitu Chid anatumia, kwa hiyo ametengenezea ubaya Chid kadata, madawa yamempeleka pabaya,” ameongeza Chid.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.