Aliyemuita Kafulila Tumbili Yeye Ndiye Tumbili – Rais Magufuli

Rais wa Jamuhuri wa Muungano Wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amempongeza aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila kutokana na namna alivyojitoa katika kutetea maslahi ya Watanzania kwenye sakata la Escrow.

Rais Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Nguruka katika hafla ya uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji uliopo Tarafa ya Nguruka katika Wilayani Uvinza ambapo alisema kuwa akiondoka hapo bila kumpongeza Kafulila atakuwa amefanya dhambi.

“Natambua kwamba Kafulila yupo chama kingine, lakini kwenye suala la IPTL, aliweka maslahi ya Taifa mbele na kusimamia ukweli hivyo nampongeza na pongezi hizo ni za dhati kwani zinatoka moyo. Wizi uliokuwa unafanywa na IPTL ni mkubwa hivyo Kafulila alisimama kutetea umma wa watannzani.

“Wakamtisha wengine kumpeleka mahakamani, wakamtukana wee, wengine wakamuita tumbili, sasa tumbili amefanya makubwa kwa ajili ya Watanzania. Wao ndio matumbili, huyu Kafulila alifanya kazi ya Mungu ya kuwatumikia Watanzana,” alisema Rais Magufuli huku wakazi wa eneo hilo wakilipuka kwa furaha.

Na Emmy Mwaipopo

Chanzo: Bongo5

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.