Alikiba na Nandy wang’ara tuzo za AFRIMA 2017

Usiku wa kuamkia leo nchini Nigeria kulitolewa tuzo za All Africa Music Awards 2017 (AFRIMA) ambapo wasanii wawili kutoka Bongo, Alikiba na Nandy wameibuka washindi.

Alikiba ameshinda Tuzo mbili katika vipengele vya Best Africa Collaboration kupitia ngoma ‘Aje’ pamoja na kipengele cha Best Artist or Group in Africa RnB and Soul ambapo pia ni kupitia ngoma ya ‘Aje’ kwa kushirikiana na M.I.

Wakati huo Nandy akishinda katika kipengele cha Best Female Artist In Eastern Africa Award. Wasanii wengine wa Tanzania waliokuwa wakiwania ni pamoja na Feza Kessy na Vanessa Mdee.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.