Alichosema Nape Nnauye kuhusu Lissu

Aliyekua Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amefunguka na kumuombea Mbunge Tundu Lissu ili aweze kupona na kuja kueleza ukweli juu ya watu ambao wamemfanyia kitendo hicho cha kinyama.

 Mbunge wa Mtama Nape Nnauye na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu walipokutana jana kabla ya mbunge huyo kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Nape Nnauye jana kabla ya Tundu Lissu kupigwa risasi majira ya saa 7 mchana anadai alikutana naye na kuongea naye katika viwanja vya bunge na baadaye kuja kupata taarifa kuwa amepigwa risasi na watu wasiojulikana.

“Masaa machache kabla ya kushambuliwa kwa risasi jana! Naamini mjomba utarudi utueleze ukweli wa wauaji hawa! Hasa ‘the T460CQV’ uliyoilalamikia” aliandika Nape Nnauye kweye mitandao yake ya jamii.

Mpaka sasa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu yupo nchini Kenya akipatiwa matibabu kufuatia majeraha ambayo ameyapata katika mwili wake

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.