ALEXIS SANCHEZ APANGA KUONDOKA ARSENAL.

Ni Baada Ya Kipigo Cha Goli 5-1 Kutoka Kwa Bayern Munich UEFA

0

Mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Chile, Alexis Sanchez yupo mbioni kuachana na klabu yake ya Arsenal kufuatia kipigo cha mbwa walichokipata kutoka kwa Bayern Munich ya Ujerumani cha magoli matano (5) kwa moja (1)  kwenye mchezo wa UEFA wa Februari 15 mwaka huu.

Kulizuka kulalamikiana na kutupiana lawama baina yawachezaji wa Arsenal kutokana na kipigo hicho, huku ikiropotiwa kocha msaidizi wa klabu hyo, Steve Bould akipatwa na hasira kupelekea kuutupia ukuta chupa ya maji.

Mashabiki wa arsenal walionekana wakijadiliana na kuhojiana kuhusu hatima ya kocha Arsene Wenger ndani ya klabu hyo, lakini Wenger mwenyewe amepinga kuwepo lawama baina ya wachezaji wake na kusema kwamba hali ni shwari ndani ya klabu ya Arseanal ya jijini London, Uingereza.

Zimekuwepo ripoti kadhaa kuhusu mkataba wa Sanchez kuichezea timu hyo mpaka mwisho wa msimu, inasemekana kwamba mshambuliaji huyo anaweza kuondoka kutokana na kuwepo na kipengele katika mkataba wake kinachomruhusu kuondoka katika hatua ya kwanza ya mtoano ya mashindano ya UEFA.

Katika pambano hilo Sanchez alikosa penati mapema dakika ya 30 ya mchezo kabla ya kuifungia Arsenal bao pekee.

 

Miamba ya Ufaransa PSG na vianara wa ligi ya Italia(SrieA), Juventus ni timu zinazohusishwa na kuhitaji huduma ya Sanchez aliyefunga magoli 17 pamoja na kutengeneza magoli 8 ligi kuu ya Uingereza, EPL

Hatima ya kocha Arsene Wenger ambaye mitazamo yake imewagawa katika makundi mashabiki wa Arsenal inatazmiwa kupatikana kipindi cha kiangazi, huku kipa wa zamani wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Ujerumani Jens Lehaman anapendekeza inambidi Sanchez awe muwazi.

”Nafikiri Sanchez anahitaji kuwa muwazi, kama anapanga kusaini mkataba mpya afanye hivyo sasa hivi. Pia kama hana mpango wa kusaini mkataba mpya afanye maamuzi mapema ili kila mtu afahamu ni kitu gani kinaendelea.”  Alinukuliwa Jens Lehaman akihojiwa na  TalkSport.

Kesho jumatatu Arsenal watakutana na Sutton ikiwa ni mckezo wa mashindano ya kombe la FA la Uingereza.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.