Ajuza ambaye amehitimu shahada akiwa na miaka 91

Ajuza mweye umri wa miaka 91 kutoka nchini Thailand amepata shahada yake baada ya masomo yaliyomchukua karib

Kimlan Jinakul amekuwa na ndoto wa kujiunga na chuo kikuu tangu awe mtoto lakini hakupata fursa hiyo.

Lakini miaka mingi baadaye baada ya kuwasomesha watoto wake hadi viuo vikuu, aliamua kujiunga na chuo na siku ya Jumatano amefanikiwa kupata shahada yake.

Kimlan Jinakul with familyWatu wa famila yake walidhuria sherehe za kuhitimu kwake

Kimlan ambaye anatokea mkoa wa Lampang kaskazini mwa Thailand. Alikuwa mwanafunzi mwenye kuelewa masomo na alisomea kati ya shule bora zaidi mkoani humo.

Lakini hakufanikiwa kuendelea hadi chuo kikuu wakati huo na baada ya familia yake kuhamia mji wa Bangkok, aliolewa na kaachana na ndoto yake ya kusoma zaidi.

Watoto wake wanane kati ya watano wana shahada za uzamili na hata mmoja amefanikwa kupata shahada ya uzamifu au PhD nchini Marekani.

Juasiripukdee familyIlimchukua Kimlan zaidi ya miaka 10 kupata shahada

Wakati mmoja wa mabinti zakae ambaye alikuwa akifanya kazi hospitalini alianza kusoma katika chuo cha Sukhothai Thammathirat naye aliamua kujiunga.

Alikuwa na umri wa miaka 72 wakati alijiunga na chuo kiuu, lakini kufuatia kifo cha moja wa mabinti zake aliacha masomo kwa miaka kadha.

Akiwa na umri wa miaka 85 alirudi shuleni tena na kuendelea na masomo.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.