Ajali mbaya ya lori na basi yaua na kujerui 32 iringa

0

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 32 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la Vitu Laini linalofanya safari zake kutoka vijiji vya Kilolo kwenda Iringa Mjini kugongana na lori la mbao karibu likiwa limekaribia kufika Iringa Mjini.

Akizungumza  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Peter Kakamba amethibitisha kutokea kwa ajli hiyo na kueleza kuwa majeruhi wote wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa.
“Ni kweli ajali imetokea leo asubuhi nje kigogo ya Mji wa Iringa, basi ndilo limelogonga lori kwa nyuma na kusababisha kifo cha mtu mmoja aliyeaga dunia palepale na kusababisha majeruhi 32.

“Majeruhi wote tumewapeleka katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa ambako wanaendelea kupatiwa matibabu mpaka sasa.
Alisema Kamanda Kakamba.Kuhusu chanzo cha ajali hiyo haijafahamika kama ni matatizo ya gari au mwendoksasi wa dereva hivyo Kamanda Kakamba amesema watatoa taarifa rasmi baabdaye kuhusu tukio hilo.

Facebook Comments

You might also like More from author

Leave A Reply

Your email address will not be published.